Msanii wa kuigiza Ayoub ambaye katika tamthilia ya 'Jambo na vijambo'
anaigiza kama Yesu amefunguka na kusema kuigiza kama Yesu katika
tamthilia hiyo inamletea shida kwa baadhi ya watu ambao siyo waelewa.
Ayoub alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNewz na kudai
kuwa kuna wakati hata majirani waligombana na mkewe na hawakutaka
kusemeshana naye kwa kuwa mumewe anamuuigiza 'Yesu'
"Hata mke wangu kishagombana na watu kwa sababu tu ya mimi kuigiza kama
Yesu, wanamwambia mumewe anamgeza mtume wetu Yesu wetu kwa hiyo
usinisemeshe, mke wangu akaja kunipa mimi hizo habari nikabaki kucheka
tu, lakini katika ule u serious zaidi sijaona kama kumetokea tatizo
kubwa mimi ni muislam lakini yapo makanisa yananiita nikawasaidie
kutengeneza kazi ya sanaa baada ya kuniona kwenye kile kipindi, kwa hiyo
wenyewe wakristo ambao wamezama kwenye imani kuniona naigiza kama Yesu
hawafikirii vibaya sababu hata nachoigiza mle ndani kinaendana na yale
aliyokuwa anatenda Yesu, hivyo huwezi kuona amefanya jambo lolote baya
yule muhusika wa Yesu ambaye ni mimi" alisema Ayoub
Mbali na hilo Ayoub anasema watu ambao wanakuwa na mtazamo hasi juu ya
uhusika wake kama Yesu ni wachache sana ukifananisha na wale ambao
wanafurahia kwani mambo mengi ambayo anafanya muhusika ni mambo ya
msingi.
"Hata ukiangalia kwenye ukurasa wa facebook wa EATV tukiweka post
akitokea mtu ambaye atazungumza vibaya juu ya 'character' Yesu wapo watu
wengine wanakuja kumsema sana na kumuelewesha vizuri juu ya uhusika wa
Yesu, kwa hiyo utaona watu wanaozungumza uzuri wanashinda kutokana na
mazuri ambayo muhusika amefanya" alisema Ayoub
Kipindi cha Jambo na Vijambo kinaruka kila Jumapili kuanzia saa 12:30 jioni katika ting'a namba moja kwa vijana EATV
Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Showing posts with label UDAKU. Show all posts
Saturday, July 08, 2017
JACK Wolper Aweweseka Juu ya Mpenzi Wake Mpya
Written by
1:51:00 AM

Staa huyo alituma dongo hilo kupitia
mtandao wake wa Snapchat, ambapo alikuwa akisema kuwa, anatamani sana
kumuweka hadharani mpenzi wake huyo mpya lakini anaogopa kunyakuliwa
tena na wakware wa kizungu kama alivyofanyiwa kwa mpenzi wake aliyepita
ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva.
Star Mix hili lilimtafuta Wolper
ambaye baada ya kubanwa kutaka kujua jina la bwana huyo aliyenaye
alianza kwa kuangua kicheko na kusema kuwa kuna wakati mwingine mtu
anazungumza kufurahisha watu wacheke lakini si kwamba kuna mtu kweli kwa
sasa.
“Jamani kuna kipindi mtu unawafanya watu wafurahi na kucheka sio kila unachozungumza mtu kiwe cha kweli.”
Category :
UDAKU
Jini Kabula Adaiwa Kuzua Timbwili Hotelini
Written by
1:48:00 AM

MSANII wa filamu Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ juzikati alidaiwa kuzua timbwili la aina yake kwenye Hoteli ya Lamada iliyopo Ilala jijini Dar baada ya tatizo alilolipata siku chache zilizopita la kudata kiakili kudaiwa kujirudia.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichokuwepo hotelini hapo, mwanadada huyo alienda Lamada kumfuata msanii mwenzake Esha Buheti ambaye ndiye shosti wake mkubwa kwa sasa lakini alipoambiwa hayupo, ndipo alipowaanzishia timbwili wahudumu.
“Alizua timbwili la aina yake, ikabidi watu waliokuwa eneo la tukio wafanye kazi ya ziada kumtuliza.
“Baadaye ikabidi wamdanganye kwamba Esha yupo Muhimbili kapelekwa kujifungua, ndipo akacharuka tena akitaka apelekwe hukohuko akamuone, hawakumpeleka ila waliamua kumpakiza kwenye gari na kumzungusha maeneo mbalimbali ya jiji ili awe sawa,” alidai sosi huyo. Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kuona ana nafuu kidogo waliamua kumpeleka Mbagala ambako ndiko ndugu zake waliko.
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, paparazi wetu alimvutia waya mtu wa karibu na Kabula ambaye ni mzazi mwenziye, Tuesday Kihangala `Mr. Chuz’ ambaye alieleza kuwa, amepewa taarifa na ndugu wa mwanadada huyo kwamba bado hayupo sawa kiakili na anatafakari jinsi ya kumsaidia ili aweze kupona kabisa. “Leo (juzi) hii ndugu zake wamenitaarifu kwamba bado hajawa sawa na hali yake inawachanganya sana, walinipa niongee naye ili niamini, yaani anaongea maneno mengi mfululizo, kwa kweli anahitaji matibabu ya kina kabla ugonjwa haujakolea,” alisema Chuz.
Jini Kabula hivi karibuni alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akidaiwa kuchanganyikiwa akili lakini siku chache baadaye alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kabla ya juzi mambo kudaiwa kuharibika tena.
Source: Global Publisher
Category :
UDAKU
Subscribe to:
Posts (Atom)


