Msanii wa kuigiza Ayoub ambaye katika tamthilia ya 'Jambo na vijambo'
anaigiza kama Yesu amefunguka na kusema kuigiza kama Yesu katika
tamthilia hiyo inamletea shida kwa baadhi ya watu ambao siyo waelewa.
Ayoub alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha eNewz na kudai
kuwa kuna wakati hata majirani waligombana na mkewe na hawakutaka
kusemeshana naye kwa kuwa mumewe anamuuigiza 'Yesu'
"Hata mke wangu kishagombana na watu kwa sababu tu ya mimi kuigiza kama
Yesu, wanamwambia mumewe anamgeza mtume wetu Yesu wetu kwa hiyo
usinisemeshe, mke wangu akaja kunipa mimi hizo habari nikabaki kucheka
tu, lakini katika ule u serious zaidi sijaona kama kumetokea tatizo
kubwa mimi ni muislam lakini yapo makanisa yananiita nikawasaidie
kutengeneza kazi ya sanaa baada ya kuniona kwenye kile kipindi, kwa hiyo
wenyewe wakristo ambao wamezama kwenye imani kuniona naigiza kama Yesu
hawafikirii vibaya sababu hata nachoigiza mle ndani kinaendana na yale
aliyokuwa anatenda Yesu, hivyo huwezi kuona amefanya jambo lolote baya
yule muhusika wa Yesu ambaye ni mimi" alisema Ayoub
Mbali na hilo Ayoub anasema watu ambao wanakuwa na mtazamo hasi juu ya
uhusika wake kama Yesu ni wachache sana ukifananisha na wale ambao
wanafurahia kwani mambo mengi ambayo anafanya muhusika ni mambo ya
msingi.
"Hata ukiangalia kwenye ukurasa wa facebook wa EATV tukiweka post
akitokea mtu ambaye atazungumza vibaya juu ya 'character' Yesu wapo watu
wengine wanakuja kumsema sana na kumuelewesha vizuri juu ya uhusika wa
Yesu, kwa hiyo utaona watu wanaozungumza uzuri wanashinda kutokana na
mazuri ambayo muhusika amefanya" alisema Ayoub
Kipindi cha Jambo na Vijambo kinaruka kila Jumapili kuanzia saa 12:30 jioni katika ting'a namba moja kwa vijana EATV
Saturday, July 08, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments: